Joto litapanda zaidi kuliko kawaida katika Pembe ya Afrika
2024-08-30 09:29:55| CRI

Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa ICPAC kilicho chini ya Jumuiya ya Maendeleo ya Kiserikali ya Afrika Mashariki IGAD kimesema ukanda wa Pembe ya Afrika utakuwa na joto kali zaidi kuliko kawaida kuanzia Septemba hadi Novemba.

ICPAC imebainisha katika utabiri wake mpya kwamba joto katika baadhi ya nchi linaweza kupanda hadi zaidi ya nyuzi joto 34. Imesema ukame utakuwa mkali zaidi kuliko kawaida katika maeneo ya mashariki ya ukanda huo katika msimu wa Septemba hadi Novemba huku joto likiwezekana kuwa kubwa katika sehemu nyingi.

Kituo hicho cha IGAD pia kilitabiri mvua zitakuwa nyingi kuliko kawaida katika baadhi ya nchi na sehemu, zikiwemo kusini mwa Sudan, mashariki mwa Sudan Kusini, magharibi mwa Kenya, magharibi mwa Ethiopia, na baadhi ya maeneo ya Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania.