Africa CDC yasema imepata chini ya asilimia 10 ya fedha za kukabiliana na Mpox
2024-08-30 10:53:16| cri

Kituo cha Kukinga na Kudhibiti Magonjwa barani Afrika (Africa CDC) kimesema kimepokea chini ya asilimia 10 ya dola za kimarekani milioni 245 zinazohitajika kupambana na mlipuko wa Mpox katika bara hilo.

Mtendaji Mkuu wa Africa CDC Ngashi Ngongo amesema katika Mkutano wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaofanyika mjini Brazzaville, Jamhuri ya Congo, kwamba bara hilo liko chini ya shinikizo la kudhibiti mlipuko wa ugonjwa huo ambao WHO umeutangaza kuwa dharura ya afya ya kimataifa, baada ya virusi vyake kuanza kuenea kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kuingia katika nchi jirani.

Kituo hicho kimeandaa bajeti inayokadiria kiasi cha fedha kinachotakiwa na rasilimali zinazotakiwa kukusanywa ili kukabiliana na mlipuko wa Mpox barani Afrika.