Madaktari wa China watoa huduma za matibabu barani Afrika
2024-08-31 09:00:02| CRI

Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utafanyika hivi karibuni hapa Beijing. Ushirikiano wa afya ni sehemu muhimu katika ushirikiano wa kirafiki kati ya China na Afrika. Tarehe 6 Aprili mwaka 1963, kikundi cha madaktari wa China waliondoka Beijing kuelekea nchini Algeria, ikiashiria mwanzo wa China kutoa msaada wa matibabu katika nchi za nje. Katika miaka 60 iliyopita, madaktari wa China wa kizazi baada ya kizazi, wanatumia busara yao na jasho lao, hata maisha yao kusimulia hadithi zao kuhusu upendo usio na mipaka, na kuimarisha zaidi daraja la urafiki kati ya China na Afrika. 

China inatoa juhudi kutekeleza wazo la kutoa kipaumbele watu na maisha, kuzisaidia nchi za Afrika kukabiliana na magonjwa na janga la magonjwa ya kuambukiza, kujenga mfumo bora wa afya ya umma, na kutumia vitendo halisi kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya pamoja ya afya kati ya China na Afrika. Katika kipindi cha Ukumbi wa Wanawake leo hii tutaangalia jinsi madaktari wa China wanavyofanya kazi katika nchi za Afrika na changamoto wanazokumbana nazo.