Mtafiti katika Taasisi ya Elimu ya Sera katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa nchini Ethiopia, Balew Demissie amesema, ushirikiano kati ya China na Afrika umeshinda majaribu ya muda katika mazingira ya kimataifa yanayobadilika na kuzidi kusonga mbele.
Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua siku chache kabla ya Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika utakaofanyika wiki hii hapa Beijing, Mtafiti huyo amesema urafiki kati ya pande hiozo mbili umeshuhudia mabadiliko mengi ya kihistoria pamoja na changamoto mbalimbali.
Amesema uhusiano kati ya China na Afrika unatokana na urafiki wa pande mbili, uhusiano wa pande nyingi na wa kina, unaojumusiha ushirikiano katika maeneo mengi ikiwemo maendeleo ya uchumi, biashara, utamaduni, elimu, afya, siasa, uongozi, usalama, diplomasia na mahusiano ya watu na watu.
Bw. Demissie amesema, biashara kati ya pande hizo mbili imekua kwa kiasi kikubwa na kuifanya China kuwa mwenzi mkubwa wa biashara wa Afrika kwa miaka mingi, na kufungua masoko na fursa mpya kwa nchi zinazoibuka barani Afrika.