Wizara ya Afya ya nchini Sudan imesema, mvua kubwa na mafuriko vimesababisha vifo vya watu 173 na kujeruhi wengine 505 tangu kuanza kwa msimu wa mvua mwezi Juni mwaka huu.
Ripoti iliyotolewa jumamosi na Wizara hiyo imesema, mafuriko hayo yameathiri zaidi ya watu 170,000 katika mikoa 11 kati ya 18 nchini Sudan, kubomoa nyumba 18,665 na nyingine 14,947 zimeharibika.
Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) limetangaza hivi karibuni, kuwa limeanza kugawa msaada wa chakula katika mkoa wa Darfur nchini Sudan, ambapo malori yaliyobeba tani 1,134 za chakula yaliingia nchini humo kutokea Chad.