Raia wa Israel wafanya maandamano na kutoa wito wa kusimamisha mapambano
2024-09-02 08:56:17| cri


Raia wengi wa Israel jana wamefanya maandamano na kuitaka serikali ya nchi hiyo ifikie makubaliano ya kusitisha mapambano na kundi la Hamas, na kuhimiza kuachiliwa huru kwa Waisrael waliofungwa kwenye Ukanda ya Gaza.

Mapema jana, Jeshi la Israel lilitangaza kugundua miili ya Waisrael sita waliofungwa kwenye Ukanda wa Gaza, taarifa iliyoamsha hasira ya watu nchini Israel.