Rais Xi Jinping wa China leo Jumatatu amekutana na Rais wa Mali Assimi Goita, ambaye yuko Beijing kwa ajili ya Mkutano wa Kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).
Viongozi hao wawili kwa pamoja wametangaza kuinua uhusiano baina ya nchi hizo mbili hadi kuwa ushirikiano wa kimkakati.
Katika mkutano huo, Rais Xi amesema China inapenda kukuza urafiki wa jadi na Mali, kuendelea kusaidiana kithabiti, na kutoa msaada kadiri ya uwezo wake kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi ya Mali na kuboresha maisha ya watu.