Moja ni nchi kubwa zaidi inayoendelea, na jingine ni bara lenye mkusanyiko mkubwa wa nchi zinazoendelea. Uzoefu wao unaofanana wa kihistoria na matarajio ya maendeleo ya pamoja yamezifanya China na nchi za Afrika kuwa marafiki wa karibu, washirika wazuri, na ndugu wa kweli ambao wapo pamoja kwenye dhiki na faraja.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na CGTN na Chuo Kikuu cha Renmin cha China kupitia Taasisi ya Mawasiliano ya Kimataifa katika Zama Mpya kwa wahojiwa wa Afrika, asilimia 90.4 ya wahojiwa hao wanaamini kuwa vitendo na kanuni za ushirikiano kati ya China na Afrika vimeweka mfano kwa nchi zinazoendelea katika masuala ya kimataifa na kutoa suluhisho muhimu kwa ajili ya kurekebisha mfumo wa utawala wa kimataifa.
Katika utafiti huo, asilimia 81.7 ya wahojiwa wanaamini kuwa China daima imekuwa ikitoa heshima, uungaji mkono wa pande mbili na usaidizi kwa Afrika.
Asilimia 80.9 ya wahojiwa wanashukuru kwamba China imekuwa ikichukulia ushirikiano wake na nchi za Afrika kama msingi wa sera ya mambo ya nje ya China. Asilimia 86.3 ya wahojiwa wanathamini sana kanuni ya China ya udhati, matokeo halisi, upendo na nia njema, na kutarajia kujenga jumuiya iliyo karibu zaidi kati ya China na Afrika yenye mustakabali wa pamoja katika zama mpya.
Wakati huohuo, asilimia 88.9 ya wahojiwa wanaamini kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika umeboresha hali ya jumla ya kiuchumi na kijamii barani Afrika, na kuleta manufaa yanayoonekana kwa watu wa Afrika. Miongoni mwao, asilimia 91.6 wanaamini kuwa ushirikiano kati ya China na Afrika umeboresha miundombinu ya Afrika, huku asilimia 74.6 wakihisi kuwa umeongeza viwango vya maisha.
Utafiti huu wa maoni ya umma ulifanywa kwa wahojiwa 10,125 kutoka nchi kumi za Afrika zikiwemo Cameroon, Botswana, Misri, Ethiopia, Ghana, Kenya, Morocco, Nigeria, Afrika Kusini na Tanzania.