Kenya yaadhimisha Siku ya Tiba ya Jadi ya Afrika kwa kutoa wito wa kutambuliwa kwa tiba hiyo
2024-09-02 08:56:54| CRI

Siku ya Tiba ya Jadi ya Afrika mwaka 2024 imeadhimishwa katika jiji la Nairobi nchini Kenya jumamosi iliyopita na kutoa wito wa kujumuisha tiba ya jadi katika mfumo mkuu wa matibabu.

Watunga sera, wanasayansi, na wataalamu wa tiba ya jadi walihudhuria tukio hilo lililokuwa na kaulimbiu ya “Kuunga mkono upatikanaji wa tiba bora na salama ya jadi kupitia mfumo sahihi wa usimamizi.”

Mkuu wa Idara ya Dawa Mbadala na za Asili katika Wizara ya Afya nchini Kenya Pauline Duya amesema, Kenya imejizatiti kuboresha matumizi ya dawa hizo katika tiba na udhibiti wa magonjwa sugu.

Siku ya Tiba za Asili barani Afrika inaadhimishwa kila Agosti 31, na inalenga kutambua nafasi muhimu ya dawa za asili katika kudumisha mahitaji ya afya ya msingi, ikiwemo kutibu magonjwa ya kuambukiza na yasiyo ya kuambukiza.