Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye amekuja China kushiriki katika Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) hapa Beijing.
Marais hao wawili wametangaza kuwa, uhusiano kati ya pande hizo mbili umeboreshwa kuwa uhusiano wa kiwenzi na ushirikiano wa kimkakati kwa pande zote katika zama mpya.
Katika mazungumzo hayo rais Xi ameeleza kuwa, China na Afrika Kusini kuimarisha mshikamano na ushirikiano kunalingana na matarajio ya pamoja ya watu wa pande hizo mbili, na mchakato wa kihistoria ya Dunia ya Kusini kujiendeleza na kupata ustawi, na kuna umuhimu mkubwa wa kizama na ushawishi wa dunia.
Naye Rais Ramaphosa amesema Afrika Kusini iko tayari kushirikiana na China kupanua ushirikiano wa kiutendaji katika sekta za uchumi na biashara, miundo mbinu, nishati mpya na kupunguza umaskini, kuimarisha mawasiliano ya utamaduni na ushirikiano wa elimu na utamaduni, na kuhimiza uhusiano kati ya pande hizo mbili kupata mafanikio makubwa zaidi, pia kusaidia Afrika Kusini kutimiza mambo ya kisasa.