Takwimu zilizotolewa na Idara ya Forodha nchini China zimeonyesha kuwa, nchi hiyo imeendelea kuimarisha biashara na nchi za Afrika katika miaka ya karibuni, huku kukiwa na ongezeko kubwa la biashara kati ya pande hizo mbili.
Kwa mujibu wa Idara Kuu ya Forodha ya China, kuanzia mwaka 2000 hadi mwaka jana, ukubwa wa biashara kati ya China na Afrika uliongezeka kutoka chini ya dola za kimarekani milioni 14.08 hadi dola za kimarekani bilioni 280, huku ukuaji wa kila mwaka ukifikia asilimia 17.2.
Katika kipindi cha mwezi Januari hadi Julai mwaka huu, biashara kati ya China na Afrika iliongezeka kwa asilimia 5.5 na kufikia kiwango cha juu katika historia ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka jana.
China imejikita kwa muda mrefu katika kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara na nchi za Afrika, na uhusiano wa kiviwanda kati ya pande hizo mbili umeendelea kuwa wa karibu zaidi.