Rais wa Kenya asema FOCAC imesaidia nchi nyingi za Afrika kuelekea kwenye usasa
2024-09-03 08:56:23| cri

Rais wa Kenya William Ruto amesema Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wa mwaka huu utaonyesha mwelekeo wa ushirikiano kati ya Afrika na China katika enzi mpya, kuhimiza ukuaji wa uchumi wa kijani, kuhimiza maendeleo ya amani, na kuimarisha kujifunza kwa pamoja kati ya ustaarabu.

Akizungumza katika mahojiano na Shirika la Habari la China Xinhua katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Rais Ruto amesema, Kenya inaamini kwamba Baraza hilo litaongeza msukumo mpya katika ushirikiano wa Kenya na China na kusaidia Kenya na nchi nyingi za Afrika kuelekea usasa.

Rais Ruto amesema, China na Afrika zimeweka utaratibu thabiti kupitia FOCAC ili kufanya mazungumzo na kukuza maendeleo ya maelewano kati ya pande hizo mbili katika masuala ya usalama, utamaduni, kilimo, viwanda na maendeleo na nyanja zingine.

Pia amesema, ushirikiano wa kimkakati kati ya Kenya na China unaendelea kusonga mbele, na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili uko mstari wa mbele katika ushirikiano wa Afrika na China.