Afrika yakabiliwa na shinikizo kubwa kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa
2024-09-03 09:01:03| cri



"Ripoti ya Hali ya Hewa ya Afrika ya 2023" iliyotolewa jana na Shirika la Hali ya Hewa Duniani imesema, Afrika inakabiliwa na shinikizo kubwa linalotokana na mabadiliko ya hali ya hewa na kubeba gharama kubwa "isiyo na uwiano" katika kukabiliana na hali ya hewa. 

Ripoti hiyo imeonyesha kuwa nchi za Afrika hupoteza wastani wa asilimia 2 hadi 5 ya pato la taifa (GDP) kila mwaka kutokana na hali mbaya ya hewa, na nchi nyingi za Afrika hutumia kiasi cha asilimia 9 ya bajeti zao kukabiliana na hali mbaya ya hewa.