Uwanja wa Arusha unaojengwa na kampuni ya China utakuwa mwenyeji wa fainali za AFCON 2027
2024-09-04 23:02:03| cri

Serikali ya Tanzania imethibitisha kuwa Uwanja wa soka wa Arusha unaojengwa na Kampuni ya Ujenzi na Uhandisi wa Reli ya China (CRCEG), ambayo viongozi wake wameahidi kujenga kituo cha kisasa, utakamilika kwa wakati kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027, zitakazoandaliwa na Tanzania, Kenya na Uganda.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania Dk. Damas Ndumbaro, amesema hatua za awali ya ujenzi wa uwanja huo zimefikia asilimia tano, ambazo ni pamoja na maandalizi ya eneo, manunuzi na ujenzi wa ofisi za mkandarasi.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa mechi za AFCON kwenye Uwanja wa Benjamin William Mkapa jijini Dar es Salaam, Amaan Complex mjini Zanzibar, na Uwanja unaoendelea kujengwa Arusha.

Uwanja huo mpya utakuwa na uwezo wa kupokea watu 30,000 na utakuwa wa kisasa zaidi Afrika Mashariki. Mbali na mechi za ndani na nje ya uwanja huo pia kutakuwa na shughuli mbalimbali za riadha na biashara na kuinua kwa kiasi kikubwa shughuli za utalii.