Marais wa China, Tanzania na Zambia washuhudia utiaji saini Mkataba wa kufufua reli ya TAZARA
2024-09-04 14:35:21| cri

Rais wa China Xi Jinping, Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zambia Hakainde Hichilema kwa pamoja wameshuhudia utiaji saini waraka wa maelewano kuhusu mradi wa ufufuaji wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA).

Samia na Hichilema wako Beijing kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wa mwaka 2024.