Mkutano wa tisa wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ulifanyika jana hapa Beijing, ambao umefanya maandalizi ya pande zote kwa mkutano wa kilele wa Baraza hilo unaoanza leo Septemba 4.
Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, kauli mbiu ya mkutano huo wa kilele ni “Kushirikiana kuelekea kuwa nchi za kisasa, na kujenga kwa pamoja jumuiya ya kiwango cha juu yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika”, ambayo inafuata matakwa ya lazima ya maendeleo ya historia na kuonesha matarajio ya pamoja ya watu wa China na Afrika. Ameongeza kuwa, rais Xi Jinping wa China atashirikiana na viongozi wa nchi za Afrika kuweka mpango mpya wa uhusiano kati ya China na Afrika, na kuelekeza mwelekeo wa maendeleo ya “Dunia ya Kusini”.