Ashley Griffith, mwenye umri wa miaka 46, amekiri makosa ya kubaka na kudhalilisha wasichana wadogo waliokuwa chini ya uangalizi wake katika vituo vya kulelea watoto nchini Australia kwa zaidi ya miaka 20.
Griffith amekiri kutenda makosa 307 katika vituo vya kulelea watoto huko Brisbane na Italia kati ya mwaka 2003 na 2022. Tuhuma hizi zinamhusisha Griffith na udhalilishaji wa watoto wengi, hasa wasichana waliokuwa chini ya umri wa miaka 12.
Polisi nchini Australia wamesema kwamba Griffith ni miongoni mwa washtakiwa waliokuwa wakitafutwa kutokana na vitendo vya udhalilishaji wa watoto nchini humo.