Wafungwa 129 wameuawa na wengine 59 kujeruhiwa katika jaribio la kutoroka katika Gereza la Makala lililopo Kinshasa, mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mapema jumatatu wiki hii.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama Jacquemain Shabani amesema jengo la utawala, usajili, zahanati, na maghala ya chakula vilichomwa moto wakati wa tukio hilo.
Mwezi Julai mwaka huu, Waziri wa Sheria wa DRC Constant Mutamba aliamua kuwa wafungwa 1,284 katika Gereza la Makala wataachiliwa kwa masharti ili kupunguza msongamano wa wafungwa katika gereza hilo.