Rais Xi Jinping leo tarehe tano amehudhuria na kuhutubia ufunguzi wa Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC mjini Beijing.
Rais Xi amesema katika miaka 24 iliyopita tangu kuanzishwa kwa FOCAC mwaka 2000, China na nchi za Afrika zimeelewana na kuungana mkono, na kutoa mfano wa kuigwa kwa uhusiano wa kimataifa wa aina mpya.