Nchi za Afrika zahimizwa kuimarisha ushirikiano katika maendeleo ya mifumo ya soko la kaboni
2024-09-05 09:11:44| cri



Nchi za Afrika zinapaswa kuimarisha ushirikiano wa kikanda juu ya maendeleo ya mifumo ya soko la kaboni ili kukabiliana na changamoto zinazokabili nchi nyingi. 

Taarifa iliyotolewa jana na mkutano wa mazungumzo kati ya wataalamu kutoka Kenya, Senegal, na Zambia kuhusu kutumia masoko ya kaboni kuhimiza maaendeleo ya kijani barani Afrika, imesema nchi nyingi za Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara zinakabiliwa na changamoto katika maendeleo ya mifumo ya soko ya kitaifa, hali ambayo inaonesha haja ya uratibu.