Waziri mkuu wa Somalia Hamza Abdi Barre jana Jumatano alizindua mpango wa utekelezaji unaolenga kutafuta suluhisho kwa suala la wakimbizi wa ndani, ambalo ni moja ya changamoto zinazoikabili nchi hiyo.
Mpango huo uitwao Mpangokazi wa Suluhisho la Kitaifa (2024-2029) utatoa makazi mapya kwa watu zaidi ya milioni moja waliokimbia makazi yao, kuwezesha jamii na kuhimiza maendeleo endelevu.
Bw. Barre amesema mpango huo ni hatua muhimu katika juhudi za serikali za kutatua suala la wakimbizi wa ndani, ukilenga kuboresha maisha ya wakimbizi wa ndani zaidi ya milioni moja.