Ofisa wa Tanzania asema hatua 10 za kiwenzi kukuza uhusiano kati ya Afrika na China
2024-09-06 09:23:40| Cri

Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji na Mipango kilicho chini ya Ofisi ya Rais wa Tanzania Gilead Teri, ambaye yupo China kuhudhuria Mkutano wa Mwaka 2024 wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) amesema, Hatua 10 za Kiwenzi zilizotangazwa na Rais Xi Jinping wa China kwenye ufunguzi wa mkutano huo zitahimiza uhusiano kati ya Afrika na China kuwa na mustakabali mzuri zaidi, na anatarajia hatua hizo zitakuza ushirikiano kati ya Tanzania na China.

Teri amesema hatua hizo zinaendana na sera za uchumi na diplomasia za Tanzania, na kutokana na mfumo wa FOCAC, Tanzania na China zimefanya ushirikiano wa karibu katika sekta mbalimbali zikiwemo viwanda, mawasiliano na uchukuzi, kilimo na utalii, na ushirikiano huo umeleta manufaa ya moja kwa moja kwa Tanzania.

Amesema mchakato wa kujenga mambo ya kisasa nchini China umeonesha njia ya kujiendeleza kwa nchi za Afrika.