Peng Liyuan na wake wa viongozi wa Afrika wahudhuria mkutano kuhusu elimu ya wanawake
2024-09-06 11:27:53| cri

Peng Liyuan, mke wa Rais Xi Jinping wa China, Alhamisi alihudhuria na kuhutubia mkutano kuhusu elimu ya wanawake wa China na Afrika.

Zaidi ya wake 20 wa viongozi wa Afrika, ambao wako Beijing kuhudhuria Mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwa mwaka 2024, walishiriki kwa pamoja katika shughuli hiyo.

Katika hotuba yake, Peng alisema China na Afrika ni jumuiya yenye mustakabali wa pamoja. Wanawake wa China na Afrika kupitia kazi zao zenye bidii, hekima na za kujitolea, wameandika ukurasa mpya wa mafanikio makubwa ya mshikamano, ushirikiano na maendeleo.

Peng alisema kuwa katika kuendeleza elimu ya wanawake na kujenga mustakabali mzuri zaidi, China na Afrika zinaendana na malengo yao.

Katika mkutano huo, Marie Khone Faye, mke wa Rais wa Senegal Bassirou Diomaye Faye, na washiriki wengine pia walitoa hotuba.