Peng Liyuan akutana na mke wa rais wa Jamhuri ya Kongo
2024-09-06 15:29:27| cri

Mke wa rais Xi Jinping wa China profesa Peng Liyuan alikunywa chai na Antoinette Sassou Nguesso, mke wa rais wa Jamhuri ya Congo.

Peng Liyuan alimkaribisha Antoinette kuambatana na Rais Sassou mjini Beijing kuhudhuria Mkutano wa wakuu wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika na kufanya ziara ya kiserikali nchini China, na alikumbuka kwa furaha uzoefu usiosahaulika wa kuambatana na Rais Xi Jinping katika ziara yake nchini Jamhuri ya Kongo. Peng Liyuan amempongeza kwa juhudi za kujitolea za muda mrefu katika kukuza maendeleo ya huduma za afya barani Afrika

Antoinette ameishukuru China, hasa Peng Liyuan, kwa msaada wake mkubwa wa kuhimiza maendeleo ya shughuli za afya ya watu wa Afrika, wanawake na watoto, na kueleza nia yake ya kuimarisha zaidi mawasiliano na ushirikiano na China katika afya, elimu na nyanja nyinginezo na kutoa mchango katika kuimarisha urafiki kati ya Afrika na China.