Waziri wa mambo ya nje wa China asema mkutano wa kilele wa FOCAC wa Beijing umepata "mafanikio kamili"
2024-09-06 11:38:21| cri

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema Alhamisi kuwa Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) wa Beijing umepata mafanikio kamili.

Wang, aliyasema hayo alipokutana na wanahabari pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Senegal Yacine Fall na Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kongo Jean-Claude Gakosso.

Akifafanua kuhusu matokeo makubwa ya mkutano huo, Wang alisema uhusiano wa pande mbili kati ya China na nchi zote za Afrika zenye uhusiano wa kidiplomasia na China umepandishwa kwenye kiwango cha uhusiano wa kimkakati, na sifa ya jumla ya uhusiano kati ya China na Afrika imeinuliwa kuwa jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya hali zote katika zama mpya.

Aidha Wang alisema mapendekezo sita makuu ya kuendeleza mambo ya kisasa ya China na Afrika yametolewa. Na pia muongozo wa hatua za kuendeleza ushirikiano kati ya China na Afrika umetolewa, akiongeza kuwa Rais Xi Jinping wa China ametangaza hatua 10 za ushirikiano katika mambo ya kisasa ili kuimarisha ushirikiano kati ya China na Afrika kwa miaka mitatu ijayo.

Fall na Gakosso wameema, ushirikiano kati ya Afrika na China umebadilisha hatima ya Afrika na bila shaka utaingia katika historia kama mfano wa ushirikiano wa kimataifa.

Wamesema Afrika inapenda kushirikiana na China kutekeleza matokeo ya mkutano huo na makubaliano kati ya pande hizo mbili, kuimarisha urafiki kati ya Afrika na China, na kufikia maendeleo ya pamoja na ustawi wa pamoja.