Mwanmuziki mashuhuri duniani Diamond Platnumz amefichua kuwa ndoto yake ni kuwa tajiri namba moja duniani.
Akizungumza Jumanne, Septemba 3, 2024 wakati wa uzinduzi wa Wasafi Festival mwaka 2024, mwanamuziki huyo alisema kuwa hivi karibuni atazindua baadhi ya projekti zake zitakazompandisha hadhi na kuinua mapato yake.
“Ndoto yangu kubwa maishani ni kuwa mtu tajiri zaidi duniani. Hiyo ni ndoto yangu na ninaweza kukuhakikishia kuwa nitakuwa tajiri mkubwa zaidi duniani,” Diamond alisema.
Diamond aliwaeleza wafuasi wake kuwa hapo nyuma alitaka kumiliki gari aina ya Rolls Royce na haikuchukua muda na akalinunua, hivyo hakuna kitakachomzuia kuwa tajiri namba moja duniani.
“Na niwahakikishie kuwa nitakuwa Mtanzania ambaye ataiwakilisha nchi yake kuwa tajiri mkubwa duniani,” alisema.