Miradi ya nishati safi ya China yatarajiwa kuhimiza maendeleo barani Afrika
2024-09-09 09:10:12| CRI

Ripoti iliyotolewa na chombo cha habari cha Ujerumani Deutsche Welle inasema, miradi ya nishati safi inakuwa muhimu zaidi katika uhusiano wa kiuchumi kati ya China na Afrika, huku biashara kati ya pande hizo mbili ikishuhudia ukuaji endelevu katika miongo miwili iliyopita.

Kwenye mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika wiki iliyopita mjini Beijing, China ilitangaza mipango ya kutekeleza miradi 30 ya nishati safi barani Afrika ili kuunga mkono maendeleo ya kijani ya bara hilo. Zaidi ya hayo, China itatoa uungaji mkono zaidi wa kifedha wa dola za kimarekani bilioni 50.8 kwa nchi za Afrika katika miaka mitatu ijayo.

Kwa mujibu wa Deutsche Welle, mipango hiyo inatarajiwa kutoa nafasi mpya za ajira zaidi ya milioni moja katika nchi za Afrika.