Kamati kuu ya Chama cha kikomunisti chaChina na baraza la serikali ya China zimetuma salamu za pongezi kwa wanamichezo wa Olimpiki ya Walemavu wa China kwa mafanikio na uchezaji wao katika Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Paris ya 2024.
China ilijinyakulia medali 94 za dhahabu, 76 za fedha na 50 za shaba kwenye Michezo ya Olimpiki ya Walemavu ya Paris, na kuongoza jedwali la medali kwa mara ya sita mfululizo.