Watu 48 wafariki baada ya lori la mafuta kulipuka katikati mwa Nigeria
2024-09-09 09:10:39| CRI

Takriban watu 48 wamefariki katika ajali ya kulipuka kwa lori la mafuta kwenye barabara kuu yenye foleni huko Niger, jimbo la katikati mwa Nigeria.

Mkuu wa idara ya usimamizi wa mambo ya dharura ya jimbo la Niger Bw. Abdullah Baba-Arah, amewaambia wanahabari kuwa lori hilo liligongana uso kwa uso na lori lingine lililobeba ng'ombe kwenye barabara kuu ya Bida-Agaie-Lapai, na kusababisha lori la mafuta kulipuka.

Magari mengine mawili yalishika moto na kusababisha vifo vya watu 48. Takriban ng'ombe 50 pia walikufa kwenye tukio hilo.

Operesheni ya uokoaji ilikuwa ikiendelea ili kupata miili ya wahanga wanaoaminika kunaswa kwenye magari hayo.