Tume ya uchaguzi ya Algeria imesema, matokeo ya awali ya uchaguzi yameonesha kuwa Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria amechaguliwa tena kwa muhula wa pili.
Mkuu wa tume huru ya uchaguzi ya Algeria Bw. Mohamed Charfi amesema kwenye mkutano na wanahabari mjini Algiers, kuwa Bw. Tebboune amepata kura 5,329,253 ambazo ni sawa na asilimia 94.65 ya kura zote.
Mshindani wake wa karibu zaidi Bw. Abdelaali Hassani Cherif amepata kura 178,797 ambazo ni sawa na asilimia 3.17 ya kura zote, huku Bw. Youcef Aouchiche akipata kura 122,146.
Kwa mujibu wa tume hiyo, Baraza la katiba la nchi hiyo litapitia rufaa yoyote kutoka kwa wagombea urais kabla ya kurasimisha matokeo hayo.