Katika miaka ya hivi karibuni, kutokana na upanuzi wa ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta ya uchumi wa kidijitali, serikali za nchi za Afrika zimetambua umuhimu wa teknolojia ya dijitali katika sekta ya uchumi, na kuendelea kuongeza uwekezaji katika ujenzi wa miundo mbinu ya dijitali. Tarehe 29 Mwezi Julai mwaka huu, Wizara ya Viwanda na Teknolojia ya China (MIIT) ilitangaza kwa pamoja na mamlaka zinazohusika za nchi 26 za Afrika Mpango wa Ushirikiano wa Dijitali kati ya China na Afrika, ikiashiria kuwa Afrika itanufaishwa zaidi kutokana na teknolojia ya kidijitali.
Wakati huo huo, tangu kuzinduliwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika mwaka 2000, wanawake wengi zaidi wa China wamekwenda barani Afrika, kujishughulisha na mambo ya dijitali, kusaidia kuwaanda wataalamu wa biashara ya mtandaoni barani Afrika, na kukuza maendeleo ya biashara ya mtandaoni barani Afrika. Bibi Lei Jing, mfanyabiashara wa China nchini Kenya ambaye anawasaidia wenyeji wa huko kuanzisha biashara ya mtandaoni ni mmoja wao. Katika kipindi cha leo cha Ukumbi wa Wanawake, tutawaletea hadithi ya mfanyabiashara huyo wa China Lei Jing, na jinsi biashara hii inavyowanufaisha wanawake.