Mamlaka ya mji wa Niamey wa Niger imetoa taarifa ikisema, mji huo umezindua kampeni ya udhibiti wa mbu inayolenga kupunguza kuzaliana kwa mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa ugonjwa wa malaria umeenea sana katika maeneo yasiyo safi na yaliyo nyuma kiuchumi.
Ili kukabiliana na tishio hilo, wasimamizi wa mji huo wamewahimiza wakazi wa mji huo kuchukua hatua za lazima ya kinga, ikiwemo kulinda utoaji wa chakula na vinywaji kwa kazi za timu hizo.
Ugonjwa wa malaria unaenea kwa mwaka mzima katika maeneo yote ya vijiji na miji nchini Niger. Kwa mujibu wa maofisa wa huko, ugonjwa huo ni moja ya vyanzo vya udumavu na vifo haswa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na wajawazito.