Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bi. Mao Ning amesema China inapenda kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika katika juhudi za kuondoa mabomu yaliyotegwa ardhini katika bara hilo na kusaidia kukomesha tishio la mabomu ya ardhini haraka iwezekanavyo kupitia njia mbalimbali zikiwemo misaada ya vifaa, mafunzo ya wafanyakazi, na mwongozo wa eneo la kazi.
China imetangaza “hatua ya kufanikisha Afrika isiwe na mabomu ya kutegwa ardhini” katika mkutano wa kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika wa mwaka 2024, ambayo ni kati ya hatua mbalimbali za kutekeleza Pendekezo la Usalama Duniani barani Afrika.
Bi. Mao amesema China imechukua hatua halisi kuzisaidia Ethiopia, Angola, Eritrea, Chad na nchi nyingine nyingi kuendeleza uwezo wa kuondoa mabomu ya ardhini, kuchangia katika ulinzi wa usalama wa raia wao na kuhimiza maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika nchi hizo.