China yaunga mkono kutoa msaada endelevu wa kifedha kwenye operesheni za kulinda amani zilizoongozwa na Umoja wa Afrika
2024-09-10 11:07:02| cri

Mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Balozi Fu Cong jana alisema, China inaunga mkono kutoa msaada endelevu wa kutosha na unaokadiriwa kwenye operesheni za kulinda amani zilizoongozwa na Umoja wa Afrika.

Kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu operesheni za kulinda amani, balozi Fu amesema, kuimarisha uwezo wa Afrika katika kulinda amani na utulivu, kuongeza uungaji mkono katika mipango ya kikanda barani humo, ni mwelekeo muhimu wa Umoja wa Mataifa katika mageuzi ya kulinda wa amani.