Makampuni ya China kujenga kituo kikubwa cha umeme wa jua nchini Namibia
2024-09-10 09:04:18| CRI

Shirika la umeme linalomilikiwa na serikali ya Namibia, NamPower, limesaini makubaliano na kundi la makampuni ya China kuhusu ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme kwa nishati ya jua, chenye uwezo wa kuzalisha megawati 100, cha Rosh Pinah.

Makubaliano hayo yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 78, yatafanikisha mradi huo unaounga mkono juhudi za Namibia za kuimarisha miundombinu yake ya nishati mbadala, na unatarajiwa kuchangia kwa kiasi kikubwa usalama na malengo endelevu ya usambazaji wa umeme nchini Namibia.

Mkurugenzi Mtendaji wa Nampower Bw. Kahenge Haulofu amesema kituo hicho na miradi mingine ya miundombinu inayoendelea kujengwa, ni sehemu ya Mpango Mkakati wa Biashara wa NamPower kwa kipindi cha 2020-2025.