Ofisa mkuu mtendaji wa Reli ya Ethiopia-Djibouti Bw. Takele Uma, amesema kuunganishwa kwa reli hiyo na bandari za kimkakati nchini Djibouti kunabadilisha biashara ya kikanda na ukuaji wa uchumi.
Amesema kuunganisha reli ya kilomita 752 iliyojengwa na China na bandari za kimkakati za Djibouti, kunabadilisha biashara ya kikanda, kukuza ukuaji wa uchumi wa nchi mbili zilizounganishwa, na kuimarisha ushirikiano wa kikanda.
Amesisitiza hitaji muhimu la kupanua zaidi fursa za usafirishaji kwa kurahisisha viunganishi vya bandari na reli. Pia amesema reli hiyo iliyojengwa na China inaimarisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili za Pembe ya Afrika, na hatimaye kufungua njia ya ustawi wa pamoja.