Rwanda yaanza kujenga mji unaotumia teknolojia ya kisasa na kuhimiza uvumbuzi
2024-09-11 23:02:19| cri

Rwanda Jumanne ilianza mradi wa kujenga mji wa Kigali unaotumia teknolojia ya kisasa, mradi ambao unatarajiwa kuhimiza uvumbuzi na uwekezaji wa kimataifa nchini humo.

Kwa mujibu wa maofisa, baada ya mradi kuo kumalizika, mji huo unaotumia teknolojia ya kisasa wenye ukubwa wa hekta 61 ulioko Eneo Maalumu la Kiuchumi la Kigali huko Gasabo mjini humo, utakuwa na thamani ya dola zaidi ya bilioni mbili za kimarekani, hali ambayo inatarajiwa kuifanya Rwanda kuwa nchi kuu ya uzalishaji wa teknolojia ya kizazi kijacho.

Waziri wa teknolojia ya habari na mawasiliano na uvumbuzi wa Rwanda Paula Musoni alisema, wazo la mradi ni kuweka nafasi ya kuunganisha makampuni ya kimataifa na makampuni yanayoanzishwa hivi sasa yaliyomo ndani ya mfumo wa ikolojia ya teknolojia, ili kuyafanya yaweze kutafuta ufumbuzi kwa pamoja na kuhimiza ajenda ya teknolojia ya Rwanda.