Kikao cha 79 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa chafunguliwa
2024-09-11 09:33:08| CRI

 Mkutano wa Baraza Kuu la 79 la Umoja wa Mataifa (UNGA)  umetangazwa kufunguliwa jana Jumanne na mwenyekiti mpya wa  mkutano huo Philemon Yang.

Akihutubia ufunguzi wa mkutano , Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema Baraza Kuu ni “mahali  panakotolewa masuluhisho” kwa ajili ya kukabiliana na changamoto nyingi zinazoikabili dunia sasa, na ni nyenzo ya lazima na njia muhimu ya kuelekea mustakabali wenye amani na haki kwa watu wote.

Mwenyekiti Philemon Yang ametoa wito kwenye hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano, akihimiza ushirikiano wa kimataifa ili kutatua “masuala makubwa na yasiyo na mpaka yanayotukabili”, ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, migogoro na vurugu zinazoendelea Sudan, Haiti, Ukraine na Ukanda wa Gaza.