China yajitahidi kuisaidia Afrika kupunguza shinikizo la kulipa madeni
2024-09-11 09:15:36| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bi. Mao Ning amesema, China kamwe haitakuwa mkopeshaji mkuu barani Afrika na siku zote imekuwa ikijitahidi kuzisaidia nchi za Afrika kupunguza shinikizo la kulipa madeni yake kupitia njia za pande mbili na za pande nyingi.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Benki ya Dunia, asilimia 80 ya madeni ya nje ya Afrika yanatoka kwa wakopeshaji binafsi na wa pande nyingi, huku madeni ya pande mbili yakichukua kiasi kidogo tu.

Hata hivyo, msemaji huyo amesema, China siku zote imejitahidi kuzisaidia nchi za Afrika kupunguza shinikizo la kulipa madeni kupitia njia za pande mbili na za pande nyingi, na China ni mchangiaji mkuu wa Mpango wa Kuahirisha Ulipaji wa Madeni wa G20.