Rais Xi Jinping asisitiza kuijenga China kuwa nchi inayoongoza kielimu
2024-09-11 09:16:26| CRI

Rais Xi Jinping wa China ametaka juhudi zaidi zifanyike ili kupiga hatua halisi kuelekea lengo la kimkakati la kuijenga China kuwa nchi inayoongoza katika mambo ya elimu.

Rais Xi amesema hayo katika mkutano wa kitaifa kuhusu elimu uliofanyika Beijing kuanzia Jumatatu hadi Jumanne.

Jana Jumanne ilikuwa Siku ya 40 ya Walimu ya China. Kwa niaba ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC), Rais Xi ametoa salamu kwa walimu na wafanyakazi wengine katika sekta ya elimu kote nchini.

Rais Xi amesema iliamuliwa kuongeza kasi ya kuiboresha sekta ya elimu kuwa ya kisasa baada ya Mkutano mkuu wa 18 wa chama uliofanyika mwaka 2012, na lengo limewekwa kuijenga China kuwa nchi inayoongoza katika mambo ya elimu kabla ya mwaka 2035.

Rais Xi ameongeza kuwa, lengo hilo litahimiza juhudi za China kujijenga kuwa nchi imara na kukuza ustawi wa taifa katika pande zote kupitia mchakato wa ujenzi wa nchi ya mambo ya kisasa.