Ukarabati wa miundombinu ya TAZARA kuongeza uwezo wa kusafirisha mizigo kwa mwaka hadi tani milioni 2
2024-09-11 09:17:14| CRI

Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) imesema ukarabati wa njia ya reli kufuatia kusainiwa kwa makubaliano utaleta mabadiliko kwenye reli hiyo, na kuwa kichocheo muhimu cha maendeleo ya uchumi wa kikanda, kuendana na matarajio ya wananchi wa Tanzania na Zambia.

Kwenye taarifa yake iliyotolewa mjini Dar es salaam na makao makuu ya TAZARA, Mamlaka hiyo imesema inakadiria kuwa uwezo wa usafirishaji kwa mwaka utapanda kutoka wastani wa sasa wa tani laki 5 za ujazo hadi kufikia takriban tani za ujazo milioni 2.

Septemba 4, makubaliano muhimu kuhusu TAZARA yalisainiwa mjini Beijing, kwenye mkutano wa Baraza la Ushirikiano Kati ya China na Afrika, na kuweka alama muhimu kwa ukanda wa kati na kanda ya Afrika kwa jumla.