Kutokana na mwaliko wa Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia ambaye pia ni Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mohammed bin Salman Al Saud, Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang Jumanne aliwasili Riyadh kwa ajili ya kuendesha Mkutano wa Nne wa Kamati ya Pamoja ya Ngazi ya Juu kati ya China na Saudi Arabia na kufanya ziara nchini humo.
Li amesema anatarajia China na Saudi Arabia zitazidi kushirikiana kimkakati na kuinua kiwango cha uhusiano kati ya nchi mbili kupitia ziara yake.
Amesema urafiki wa jadi kati ya China na Saudi Arabia umekita mizizi, katika miaka 34 iliyopita tangu nchi mbili zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi, chini ya jitihada za pamoja za pande mbili, uhusiano kati ya nchi mbili umepiga hatua zaidi katika maendeleo yake, na ushirikiano wa kivitendo umepata matunda mengi.