Rais Xi Jinping wa China alifanya ziara ya ukaguzi kuanzia Jumanne hadi Jumatano kwenye mji wa Baoji mkoani Shaanxi na mji wa Tianshui mkoani Gansu, kaskazini magharibi mwa China.
Kwenye mji wa Baoji, Xi alitembelea Jumba la Makumbusho ya Vyombo vya Shaba Nyeusi ya Baoji na bustani ya ikolojia ya Mto Weihe, ambako alifahamishwa hali ya sehemu hiyo katika kuimarisha kazi ya uhifadhi na matumizi ya vitu vya kale vya utamaduni na uhifadhi wa mazingira ya kiikolojia ya Mto Weihe, ambao ni tawi kubwa zaidi la Mto Manjano.
Katika mji wa Tianshui, Xi alikagua Hekalu la Fuxi, kituo cha mashamba ya matufaa cha Nanshanl, na Mapango ya Mawe ya Mlima Maijishan, ili kuhafamishwa hali ya sehemu hiyo kuhifadhi na kurithi vitu vya mabaki ya kale vya utamaduni, na hali ya kuendeleza sekta ya uzalishaji wa kisasa wa matunda yenye sifa kipekee kwenye maeneo ya milimani.