Rais wa China atuma barua ya pongezi kwa CIFTIS
2024-09-12 14:25:41| cri

Rais Xi Jinping wa China leo ametuma barua ya pongezi kwa Maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Huduma ya China (CIFTIS) ya mwaka 2024.

Katika barua hiyo, rais Xi ameeleza kuwa, hayo ni maonesho ya kumi tangu yazinduliwe, ambayo yameonesha maendeleo yenye sifa bora ya mambo ya huduma na biashara ya huduma nchini China, na kutoa mchango katika ujenzi wa uchumi wazi wa kimataifa. Amesisitiza kuwa China inapenda kushirikiana na nchi mbalimbali duniani, kufuata mwenendo wa utandawazi wa uchumi duniani, kutumia kwa pamoja fursa, kujadiliana na kushirikiana, na kuhimiza maendeleo kwa ushirikiano, ili kuhimiza ukuaji wa uchumi wa dunia, na kuwanufaisha zaidi watu wa nchi mbalimbali duniani.