Waziri wa mambo ya nje na biashara ya kimataifa ya Zimbabwe Frederick Shava, amesema makubaliano mbalimbali yaliyosainiwa kati ya China na Zimbabwe wakati rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe alipofanya ziara ya kiserikali nchini China kabla ya mkutano wa kilele wa 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, yataimarisha ushirikiano kati ya China na Zimbabwe.
Ameeleza kuwa makubaliano ya maelewano (MoU) yaliyosainiwa kati ya nchi hizo mbili yamehusisha ushirikiano wa miundombinu, haswa ujenzi wa miundombinu katika mji mpya ulioko Mlima Hampden, na pia kuna makubaliano mengine yanayohusu kuimarisha uwezo wa Zimbabwe katika utumiaji wa nishati ya jua na ushirikiano katika kudhibiti na kutokomeza ugonjwa wa kichocho.