Wang Yi atoa wito kwa nchi za BRICS kushughulikia kwa pamoja vitisho vya usalama
2024-09-12 15:24:34| cri

Mkurugenzi wa Ofisi ya Kamati ya mambo ya nje ya China, Bw. Wang Yi jana alitoa wito kwa nchi za BRICS kushikana mikono katika kushughulikia vitisho vya usalama katika mkutano wa ngazi ya juu.

Bw. Wang amesema, katika kukabiliana na changamoto za sasa za kiusalama, nchi za BRICS zinapaswa kuwa na mtazamo wa muda mrefu, kuonyesha mtazamo wa wazi zaidi, na kushirikiana kwa karibu zaidi kushughulikia matishio ya usalama kwa pamoja, na kuingiza nishati chanya katika dunia yenye msukosuko na kutoa mchango mpya katika kujenga dunia ya amani na usalama.