Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa Baraza la 11 la Xiangshan la Beijing.
Katika barua hiyo, rais Xi ameeleza matumaini yake kuwa baraza hilo litaendelea kufuata moyo ya usawa, uwazi, ujumuishi na kufunzana, kukusanya maoni ya pamoja na kuimarisha hali ya kuaminiana, ili kutoa mchango zaidi kukabiliana kwa pamoja dhidi ya changamoto za usalama duniani na kuhimiza ujenzi wa jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.