Kampuni ya TEHAMA ya China Huawei itaunga mkono juhudi za kampuni za minara ya mawasiliano za Afrika kuongeza vyanzo anuwai vya nishati na kupunguza nyayo zao za kaboni (carbon footprint).
Ofisa mwandamizi wa Huawei Bw. Li Shaolong amesisitiza kuwa kampuni za mnara zinachukua nafasi muhimu katika ujenzi wa miundombinu ya kidijitali barani Afrika, ambayo inaonesha haja ya kuunga mkono azma zao za kupunguza utoaji wa kaboni.
Kwa mujibu wa ofisa huyo, masuluhisho ya nishati ya Huawei yamesanifiwa kutatua changamoto za nishati kupitia kutumia teknolojia za nishati mbadala kama vile nishati ya jua na kuboresha mifumo ya uhifadhi wa nishati.