Maonesho ya saba ya Kimataifa ya Viwanda ya Kenya yamefunguliwa mjini Nairobi, huku kukiwa na wito wa kuimarishwa kwa uhusiano wa kibiashara na China ili kuharakisha ukuaji wa uchumi.
Takriban washiriki 200, wengi wao wakiwa ni kutoka China, wanashiriki kwenye maonyesho ya siku tatu ya kuonyesha bidhaa mbalimbali kuanzia mashine za mashambani, vipuri vya magari, masuluhisho ya nishati mbadala, bidhaa za ngozi hadi vifaa vya kielektroniki.
Kampuni ya Afripeak Expo Kenya Limited imeandaa maonesho hayo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Uwekezaji ya Kenya (KenInvest) na Chama cha Kitaifa cha Wafanyabiashara na Wenye Viwanda cha Kenya.
Meneja mkuu wa kuhimiza Uwekezaji na Maendeleo ya Biashara wa KenInvest Bw. Pius Rotich, amesema maonyesho hayo yatasaidia kuitangaza Kenya kuwa kituo cha viwanda, biashara na ugavi.