Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema serikali imejiandaa kuongeza kwa kiasi kikubwa kiwango cha uwekezaji kwenye miundombinu nchini humo.
Rais Ramaphosa amesema hayo mjini Cape Town kwenye mkutano wa Baraza la Juu la Bunge la Afrika Kusini. Amesema uendelezaji wa miundombinu ya umma ni muhimu katika utoaji wa huduma bora na maendeleo ya kiuchumi, ndiyo maana serikali imedhamiria kuongeza kwa kiasi kikubwa kiwango cha uwekezaji katika miundombinu.
Rais Ramaphosa amekiri kuwa miradi ya miundombinu ya umma ambayo imechelewa au kutelekezwa, inadhuru uwezo wa jamii kupata huduma.